1. Tathmini ni nini?
Ni utaratibu wa kupima na
chukunguza hali halisi kwa lengo la kupata data zitakazo mwezesha mwalimu au
mtahini kufanya maamuzi yanayohusu urekebishaji au uboreshaji wa mambo mbalimbali
katika elimu.
2. Kutahini ni nini?
Ni tendo la kutoa seti ya maswali
yenye kiwango na mpangilio unaokubalika ili yajibiwe na mtahiniwa ili kupima
kiwango fulani cha elimu alichojifunza.
3. Upimaji wa
Kielimu ni nini?
Ni tendo la kutafuta ni kwa kiasi
gani mwanafunzi amepata maarifa na stadi alizofundishwa kufuatana na malengo ya
ufundishaji.
4. Mfiko ni nini?
Mfiko ni maksi inayoonesha
tofauti kati ya maksi ya juu kabisa na maksi ya chini kabisa katika seti ya
maksi za watahiniwa.
5. Ni Zana zipi
za msingi zitumikazo katika upimaji wa haraka za kufundisha na kujifunza?
Zana zitumikazo katika upimaji wa
haraka za kufundisha na kujifunza ni kama vile;
·
Maswali
·
Mazoezi
·
Majaribio na
·
Mitihani
·
Eleza kwa kifupi matumizi ya matokeo na majaribio
6. Mitihani ni upimaji
unaotolewa baada ya mwanafunzi kumaliza ngazi Fulani ya elimu. Mtihani hutolewa
katika muda maalum na muda huo hauna budi kujulikana kwa mtahiniwa.
7. Fafanua
Matumizi ya Matokeo ya Mitihani
·
Hupima na kutathmini maendeleo ya mwanafunzi katika ngazi Fulani
ya elimu.
·
Inatathmini ubora wa elimu inayotolewa
·
Inatathmini ubora wa mbinu na njia zinazotumika katika
ufundishaji
·
Hutumika katika kufanya maamuzi ya kielimu (maamuzi ya kielimu
ni kama uchaguzi kuingia ngazi nyingine ya elimu au kujifunza kozi fulani)
·
Hupima na kutathmini ufanisi wa Walimu na Mitaala
·
Husaidia kuleta ushindani katika kujifunza
8. Majaribio ni nini?
Majaribio ni maswali yanayopima
kama mada kuu iliyofundishwa imeeleweka. Majaribio yanayotolewa huwa ya masomo
mengi na hutolewa katika muda maalum kama vile mwisho wa kufundisha mada moja,
mwisho wa juma, mwisho wa mwezi au mwisho wa muhula. Lakini hutegemea zaidi na
mwalimu amejipanga vipi kufanya tahmini ya ufundishaji wa somo lake.
9. Eleza kwa
ufasaha Matumizi ya matokeo ya Majaribio
·
Humwezesha mwalimu kuona kwamba malengo ya mada zilizofundishwa
yamefikiwa.
·
Humsaidia mwalimu kujua kiwango cha uwezo wa wanafunzi katika
mada iliyofundishwa.
·
Humsaidia mwanafunzi kuweza kutafuta mbinu bora zaidi za
kujifunza na kutumia vizuri wakati (muda) wake na kupunguza kucheza.
·
Humsaidia mwanafunzi kujilinganisha na wanafunzi wenzake.
·
Husaidia kusanifu alama za mtihani wa mwisho.
·
Hutumika kurekodi maendeleo ya mwanafunzi.
10. Tunapotoa
zoezi au jaribio au mtihani, je tunapima mafanikio ya mwanafunzi au tunapima
utendaji wa wanafunzi? Eleza:
Katika ufundishaji na kujifunza
kwetu tunapima vyote viwili, mafanikio ya wanafunzi na utendaji wa wanafunzi.
Hatuwezi kutenganisha upimaji wa mafanikio na upimaji wa utendaji.
Baada ya kufundisha somo au mada
Fulani upimaji kiasi gani wanafunzi wameelewa hufanyika. Kwa maneno mengine,
tunapima wanafunzi wanaweza kufanya nini kutokana na wanavyofundishwa. Kumbuka
kuwa tunapima ngazi ya chini na ngazi ya juu za upeo wa akili (kumbukumbu,
ufahamu, uchambuzi, uunganisho na tathmini). Wakati wa kutoa ripoti za
maendeleo ya wanafunzi kwa kawaida ni vizuri kutumia utendaji wa wanafunzi.
Hatumtumii mzazi matokeo ya
mwanafunzi bali maendeleo ya utendaji.
11. Taja manufaa
ya utayarishaji wa jedwali la mtawanyo katika kutahini (table of
specification):
Manufaa ni haya yafuatayo;
·
Stadi zote zitakiwazo na jamii husisitizwa,
·
Maswali ya aina mbalimbali humsaidia mwanafunzi/mtoto kukua
kimwili, kiakili na kimwelekeo.
·
Maswali hayo hupima kwa ukamilifu zaidi maendeleo ya tendo la
kufundisha au kujifunza.
·
Utungaji wa maswali hayo mbalimbali humwongezea mwalimu upeo wa
taaluma na uthabiti wa kina chake.
·
Njia hiyo ya utungaji wa maswali inakidhi na huwakilisha mada
nyingi zaidi zilizomo katika muhtasari wa shule za msingi kwa wakati mmoja.
12. Ni mambo gani
muhimu yanayopaswa kuzingatiwa katika muundo wa mtihani?
·
Malengo ya kujifunza
·
Njia au mbinu za kujifunzia
·
Malengo ya kutahini
13. Taja aina nne
(4) za kutathmini katika Elimu.
·
Tathmini ya kupima uwezo wa kumudu kuanza masomo mapya
·
Tathmini ya kuendelea
·
Tathmini ya kudodosa
·
Tathmini ya mwisho/tamati
14. Maksi
anayopewa mwanafunzi baada ya kufanya jaribio au mtihani huitwaje?
Alama anayopata mwanafunzi hata
kabla haijarekebishwa huitwa alama ghafi
15. Taja
madhumuni manne (4) tu ya upimaji wa maendeleo ya mwanafunzi:
·
Kujua/kufahamu maendeleo ya mwanafunzi kitaaluma
·
Kubaini matatizo ya wanafunzi katika kujifunza
·
Kusaidia kupata wanafunzi wa kuendelea na masomo ya juu zaidi
·
Ni kigezo kinachotumika katika utoaji wav yeti mwishoni mwa kozi
ya mafunzo maalumu au baada ya kumaliza kiwango fulani cha elimu.
·
Taja ni hatua zipi mtafiti anapaswa kuzifuata katika kufanya
utafiti?
16. Hatua
atakazozizingatia mtafiti katika kufanya utafiti ni hizi zifuatazo;
·
Kutambua tatizo au suala la utafiti
·
Kuandika muswada wa utafiti
·
Kuandaa zana za kukusanyia data
·
Uchanganuzi na tafsiri ya data
·
Uandikaji wa ripoti ya utafiti
17. Ni mambo gani
Mtafiti anayazingatia pindi anapohitaji kufanya uchanganuzi wa data?
Katika uchanganuzi wa data
Mtafiti azingatie mambo yafuatayo;
·
Kuwepo uhusiano kati ya data na malengo
·
Kila data lazima ipate tafsiri yake
·
Kila data iwe na jibu la swali au dhanio kama lilivyokua kwenye
malengo
·
Data zichanganuliwe na kutafsiriwa kikamilifu
·
Data zinaweza kupangwa kwa kutumia chati, majedwali, grafu na
takwimu zikiambatana na maelezo, Mtafiti aeleze sababu iliyomfanya atumie aina
hiyo mahsusi ya takwimu.
18. Ni hatua
zipi mwalimu azifuate katika utungaji wa jaribio au mtihani?
Hatua zifuatazo mwalimu
analazimika kuzifuata wakati wa kutunga maswali ya mtihani;
·
Mwalimu anatakiwa kutayarisha jedwali la kutahini (table of
specification)
·
Mwalimu atunge maswali ya mtihani ikiwa utayarishaji wa jedwali
la kutahini utakua umekamilika
·
Upangaji wa maswali katika mtihani
·
Utayarishaji wa mwongozo wa usahihishaji
19. Fafanua
kwa ufasaha aina za upimaji katika Elimu ya Awali.
·
Upimaji wa awali
Upimaji huu unafanyika kabla
mtoto hajaanza shule au pale tu anapoanza shule. Unasaidia kubainisha kama
mwanafunzi ana tatizo lolote linaloweza kumzuia au kumkwamisha katika kujifunza
kwake. Pia upimaji huu utamsaidia mwalimu na mzazi kufuatilia matatizo ya
mtoto, vipaji alivyonavyo na Historia ya mtoto na familia yake.Taarifa za
upimaji huu zinaweza kutokana na hojaji za mzazi, kumchunguza mtoto na jinsi
mtoto anavyojieleza.
·
Upimaji endelevu
Upimaji huu hufanyika kwa kutumia
zana mbalimbali za upimaji, ni upimaji unaofanyika wakati mafunzo yanaendelea;
mfano mazoezi, kadi za maendeleo ya mtoto, vitabu vya kumbukumbu mbalimbali za
watoto, taarifa ya afya ya kila mwezi, mkoba wa kazi za uchunguzi wa vitendo
vya masomo na fomu ya kumbukumbu ya kazi za kila siku za mtoto.
·
Upimaji tatuzi/gunduzi
Upimaji huu nalenga katika
kutafuta kwa undani sababu zinazofanya mtoto asishiriki katika vitendo vya
ujifunzaji na michezo. Upimaji huu hufanywa wakati mwalimu anaelekeza watoto na
kuona kuwa wapo watoto ambao hawashiriki katika ujifunzaji au hawaelewi
kinachoendela wakati wa ufundishaji na ujifunzaji.
·
Upimaji tamati
Aina hii ya upimaji kwa watoto
hufanyika kwa kuunganisha taarifa zote tangu upimaji awali, endelevu na tatuzi
ili kupata taarifa sahihi ya mabadiliko ya mtoto katika nyanja zote za kiakili,
kimwenendo, afya, na ujifunzaji.Upimaji huu hufanyika mwishoni mwa mafunzo au
muhula. Lengo la upimaji tamati ni kuangalia kiwango cha mafanikio kwa ajili ya
kuendelea na mafunzo ngazi inayofuata.
Kwa kuzingatia upimaji wa
maendeleo ya mtoto katika elimu ya awali hakuna ulinganifu wa matokeo
unaofanyika wala mitihani inayotolewa kwa ajili ya kumpima mtoto. Bali upimaji
hufanyika kwa kila mtoto kulingna na maendeleo yake kwa kufuatilia mabadiliko
ya mtoto kiakili, kiafya, mwenendo na ujifunzaji tangu anapoanza mafunzo hadi
mwisho wa mafunzo.
20. Ni nini
Madhumuni na Umuhimu wa Upimaji katika Elimu ya Awali?
Madhumuni ya kupima uelewa wa
mwanafunzi katika Elimu ya Awali ni:
·
kuamsha ari ya watoto kujifunza zaidi
·
kujua maendeleo watoto kiakili, kimwenendo, kitabia na kistadi
·
kumpa mwalimu mwelekeo wa kuboresha ufundishaji
·
kutoa taarifa ya maendeleo kwa wazazi au walezi
·
kutoa taarifa za maendeleo ya elimu kwa taifa.
Sir ALMASI