Jumapili, 23 Julai 2017

Mfadhaiko (Depression) Ni Nini?




Mfadhaiko (Depression) Ni Nini?





Maana Ya Mfadhaiko Wa Akili (Depression)

Kila mmoja wetu ameshapata kuwa na huzuni wakati fulani, ni kitu cha kawaida kinachotokea wakati umepotelewa na kitu, kutokana na mihangaiko ya maisha au kutokana na kudharauiliwa. Huzuni ikizidi na ikienda kwa siku nyingi mfululizo (wiki mbili au zaidi) na ikiambatana na hali ya kujiona kuwa si wa thamani tena, kwamba ni mtu usiye na msaada wo wote – basi hii inaweza kuwa ni zaidi ya huzuni. Unaweza kuwa umepata tatizo la kiafya – mfadhaiko, ugonjwa ambao kwa bahati nzuri una tiba.
Mfadhaiko ni ugonjwa unasababisha mtu kuwa na huzuni kila wakati na kukosa hamu ya kufanya vitu au kutenda yale aliyopenda sana kufanya zamani. Mfadhaiko ni ugonjwa unaoathiri namna mtu anavyojisikia, anavyofikiri na tabia yake.
Chanzo halisi cha ugonjwa huu bado hakijafahamika. Wataalamu wanasema kuwa ni muunganiko wa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na urithi, mazingira ya maisha, mambo ambayo mtu amekutana nayo katika maisha na sababu za kisaikolojia. Mtu anaweza kukutana na jambo moja tu kubwa na baya katika maisha yake kama kufiwa na mtu wa karibu, mahusiano mabaya ya ndoa ua kubakwa na akapata mfadhaiko.
Mtu mwenye mfadhaiko hupungukiwa na uwezo wake wa kutenda kazi kiasi kwamba yeye na walio karibu naye wote huathirika.
Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wanaokunywa sana pombe au kutumia madawa ya kulevya. Watu wanaoishi na virusi vya ukimwi, wenye magonjwa ya moyo, waliopatwa na kiharusi, wenye kansa, kisukari, ugonjwa wa Parkinson’s na baadhi ya magonjwa mengine huwa kwenye hatari kubwa ya kupatwa na mfadhaiko. Mtu mwenye mfadhaiko pamoja na magonjwa hayo mengine huwa kwenye hali mabaya zaidi ya kiafya na hupata shida zaidi kuutibu ugonjwa huu.
Utafiti wa zamani ulisema kuwa watu wenye matatizo ya mfadhaiko waliathirika kutokana na kutengwa na jamii, lakini utafiti wa hivi karibuni umetoa majibu tofauti na kuonyesha kwamba mtu anatengwa na jamii kutokana na mfadhaiko alio nao.
Mfadhaiko ni ugonjwa ambao umefahamika toka zamani sana. Hippocrates aliuita ugonjwa huu Melancholia.
Watu wengi mashuhuri wameumwa ugonjwa huu na wengine katika maisha yao yote. Abraham Lincoln, raisi wa 16 wa Marekani na Winston Churchil wa Uingereza ni baadhi ya watu walioumwa ugonjwa huu katika maisha yao yote.

Aina Za Mifadhaiko Wa Akili


Tatizo hili la kuwa na mfadhaiko linakuja kwa namna nyingi. Hapa chini ni baadhi ya aina za mfadhaiko:
Major depressive disorder (major depression
Mgonjwa mwenye aina hii ya mfadhaiko anakuwa na mchaganyiko wa dalili nyingi za mfadhaiko ambazo zitamfanya ashindwe kulala, kusoma, kufanya kazi, kula na kufaidi vitu ambavyo awali vilikuwa vinamvutia sana. Aina hii ya mfadhaiko humpotezea kabisa mgonjwa uwezo wa kushiriki kwenye shughuli za kazi vizuri. Watu wengine hupatwa na hali hii mara moaja wakati wengine hurudiwa mara nyingi.
 Dysthymic disorder (dysthymia)  
Mgonjwa wa aina hii ya mfadhaiko anaweza kuwa na ugonjwa huu kwa muda mrefu, pengine miaka kadhaa, lakini hana dalili ambazo ni kali sana kama za aina ya kwanza hapo juu. Mgonjwa hufanya kazi zake ingawa si kwa ufanisi mkubwa na huwa si mtu mwenye raha kamili. Watu wengine hupatwa na hali hii mara moja tu katika maisha yao wakati wengine hurudiwa mara nyingi. Mgonjwa wa aina hii ya mfadhaiko huweza kupatwa na aina ya kwanza hapo juu mara moja au zaidi katika maisha yake.
  Psychotic depression
Endapo mfadhaiko utakuwa mkubwa na kuambatana na mtu kuwa na maluweluwe (hallucinations) na kuwa nje ya maisha halisi, mtu huyu anaweza kuwa na aina ya mfadhaiko unaoitwa Psychotic depression, ugonjwa ambao mara nyingine huitwa delusional depression.


Postpartum depression (postnatal depression)
Kama mama mzazi atapatwa na mfadhaiko wiki chache baada ya kujifungua, anaweza kuwa amepatwa na postnatal depression. Wataalamu wanasema kuwa asilimia 15 hadi 20 ya akina mama hupatwa na ugonjwa huu baada ya kujifunga, bahati mabaya ni kwamba wengi hawagunduliki na wanateseka kwa miaka mingi baada ya kujifungua. Mama anaweza kuupata ugonjwa huu muda wo wote katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya kujifungua.
SAD (seasonal affective disorder)
Idadi ya watu wanaopatwa na ugonjwa huu huoongezeka zaidi kadiri unavyokwenda mbali zaidi na Ikweta. Mwisho wa kipindi cha summer ni mwanzo wa kuona jua kwa muda mfupi zaidi au mwanzo wa saa nyingi zaidi za giza kwa siku. Mtu anayepatwa na mfadhaiko katika kipindi hiki huweza kuwa amepeta aina hii ya ugonjwa. Ugonjwa huu hutoweka wenyewe wakati wa spring au summer.
Bipolar disorder (manic-depressive illness)
Ugonjwa hauonekani kwa wingi kama aina nyingine za hapo juu. Tabia kuu ya aina hii ya mfadhaiko ni kuwa na vipindi vya dalili kuwa juu sana na baadaye kushuka. Viwango hivi vya juu na chini huitwa manias.


Dalili Za Kuwa Na Mfadhaiko

  • Kutopenda kushirikiana na watu wengine
  • Kuwa na huzuni kila wakati na kujiona kuwa ni mtu usiyefaa
  • Kukosa mwamko na hamu ya kufanya shughuli
  • Matatizo katika kufanya maamuzi
  • Kutotulia na kuwa na hasira
  • Kula zaidi au pungufu ya kawaida
  • Kulala zaidi au pungufu ya kawaida
  • Kushindwa kutuliza mawazo kwenye jambo
  • Matatizo ya kumbukumbu
  • Kutotulia na kuwa na hasira
  • kukosa raha ya maisha
  • Kukosa hamu ya kuanya mambo uliyoyapenda sana zamani na         hamu ya kufanya mapenzi
  • Kujisika vibaya juu yako au kuwa mwenye makosa
  • Kuona kwamba huwezi kutatua matatizo yako ya maisha
  • Kuumwa kichwa kubanwa misuli, matatizo ya uyeyushaji chakula tumboni, matatizo ambayo hayaponi kwa kutumia dawa
  • Kuwa na mawazo ya kujiua

Jinsi ya kutafsiri ndoto uliyoota

Katika Uislamu tumeambiwa Ndoto ni sehemu ya unabii tulioachiwa, pia uislamu unaeleza aina kuu mbili za ndoto yaani Ndoto zinazotokana na shetani na ndoto inayotoka kwa mwenyezi mungu.

Pia Uislamu umeeleza ndoto ya kweli uotwa muda gani (Mfano amesema bwana Mtume, ndoto yeyote atakayeota muumini kabla ya swala ya alfajiri, ndoto hiyo ni ya kweli), kwa ufupi ndoto ya kweli ni ile mtu anayeota usiku wa manane akiwa hana msongamano wa mawazo na wala huna janaba la hawala.

Uislamu umesema kuwa kama mmoja wenu ameota ndoto nzuri basi amfuate mmoja wenu anayejua na amweleze ili apate maana yake. Kama uislamu umeelezea vizuri kuhusu ndoto Je ndoto hutafsiriwaje?..

Kwa ufupi kuna watu wengi wanadai wana uwezo wa kutafsiri ndoto, ukweli ni kuwa utafsiri wa ndoto ni ngumu sana na hakuna mtu anyejua kutafsiri ndoto zote ukiondoa manabii ambao kwa sasa hawapo tena. Wengi wanaishia kudanganya maana halisi ya ndoto, kumbuka uislamu umesema, "KAMA MMOJA WENU AKIOTA NDOTO CHAFU NA MBAYA BASI ASIITANGAZE, MAANA NDOTO HIZO ZIMETOKA KWA SHETANI".

Leo nitawafundisha jinsi ya kutafsiri ndoto ili msije mkadanganywa na mtu lakini tafsiri nitakayowapa ni Based on Islam na sio dini nyingine, japokuwa baadhi ya ndoto inabeba maana sawa kwa muislamu na siye muislamu. Kama wanavyotafsiri wanazuoni wengine..

Ukiota ndoto yoyote katika wakati ulioelezwa basi angalia hiyo ndoto kama inafanana na Aya yeyote ya Kuran anu Hadith Yeyote ya Bwana Mtume PBUH. Hiyo itakuwa ndio maana yake:-

Mfano 1: Umeota umetumbukizwa kwenye Kisima, tafsiri yake ni surat Yusuf... Yaani Ndugu zako wanataka kukutendea uadui, lakini kwa uwezo wa Mwenyezi mungu hawatafanikiwa wanavyotaka na utakuja kuwa na uwezo wa mali na mamlaka kuliko wao.

Mfano wa Pili: Umeota ndege amekudondoshea jiwe kichwani, Tafsiri yake Surat fil... Unaonywa kuwa unafanya yaliyovuka mipaka hivyo utaangamia.

Mfano wa tatu:
Umeota Ndege anaokuambia kitu, Tafsiri yake ni surat Naml.. Habari anayokuambia ni ya kweli hivyo unatakiwa uifanyie kazi haraka.

Mfano wa nne: Umeota unakurupuka na ukaambiwa kiama!, watu wengi wanakwenda wasipopajua, Tafsiri yake ni kuwa unapewa Onyo kuna jambo linalomchukiza Mungu unalifanya acha mara moja. kumbuka pale allah aliposema kuwaambia waovu "Hakuna wanachokisubiri ila ni kiama ambacho kitawakuta Ghafla".

Inshaallah nisiwaboe kusoma ila hivyo ndivyo jinsi ya kutafsiri ndoto.... Kesho nitawaelezea maana ya kuota manabii... Ingawa kizazi cha sasa imekuwa ngumu sana mtu kuota nabiii yeyote yule..
  BY ALMASI

happy birthday sir ALMASI MICHAEL 23/JULY