Katika Uislamu tumeambiwa Ndoto ni sehemu ya unabii tulioachiwa, pia
uislamu unaeleza aina kuu mbili za ndoto yaani Ndoto zinazotokana na
shetani na ndoto inayotoka kwa mwenyezi mungu.
Pia Uislamu umeeleza ndoto ya kweli uotwa muda gani (Mfano amesema bwana
Mtume, ndoto yeyote atakayeota muumini kabla ya swala ya alfajiri,
ndoto hiyo ni ya kweli), kwa ufupi ndoto ya kweli ni ile mtu anayeota
usiku wa manane akiwa hana msongamano wa mawazo na wala huna janaba la
hawala.
Uislamu umesema kuwa kama mmoja wenu ameota ndoto nzuri basi amfuate
mmoja wenu anayejua na amweleze ili apate maana yake. Kama uislamu
umeelezea vizuri kuhusu ndoto Je ndoto hutafsiriwaje?..
Kwa ufupi kuna watu wengi wanadai wana uwezo wa kutafsiri ndoto, ukweli
ni kuwa utafsiri wa ndoto ni ngumu sana na hakuna mtu anyejua kutafsiri
ndoto zote ukiondoa manabii ambao kwa sasa hawapo tena. Wengi wanaishia
kudanganya maana halisi ya ndoto, kumbuka uislamu umesema, "KAMA MMOJA
WENU AKIOTA NDOTO CHAFU NA MBAYA BASI ASIITANGAZE, MAANA NDOTO HIZO
ZIMETOKA KWA SHETANI".
Leo nitawafundisha jinsi ya kutafsiri ndoto ili msije mkadanganywa na
mtu lakini tafsiri nitakayowapa ni Based on Islam na sio dini nyingine,
japokuwa baadhi ya ndoto inabeba maana sawa kwa muislamu na siye
muislamu. Kama wanavyotafsiri wanazuoni wengine..
Ukiota ndoto yoyote katika wakati ulioelezwa basi angalia hiyo ndoto
kama inafanana na Aya yeyote ya Kuran anu Hadith Yeyote ya Bwana Mtume
PBUH. Hiyo itakuwa ndio maana yake:-
Mfano 1: Umeota umetumbukizwa kwenye Kisima, tafsiri yake ni
surat Yusuf... Yaani Ndugu zako wanataka kukutendea uadui, lakini kwa
uwezo wa Mwenyezi mungu hawatafanikiwa wanavyotaka na utakuja kuwa na
uwezo wa mali na mamlaka kuliko wao.
Mfano wa Pili: Umeota ndege amekudondoshea jiwe kichwani, Tafsiri yake Surat fil... Unaonywa kuwa unafanya yaliyovuka mipaka hivyo utaangamia.
Mfano wa tatu: Umeota Ndege anaokuambia kitu, Tafsiri yake ni surat
Naml.. Habari anayokuambia ni ya kweli hivyo unatakiwa uifanyie kazi
haraka.
Mfano wa nne: Umeota unakurupuka na ukaambiwa kiama!, watu wengi
wanakwenda wasipopajua, Tafsiri yake ni kuwa unapewa Onyo kuna jambo
linalomchukiza Mungu unalifanya acha mara moja. kumbuka pale allah
aliposema kuwaambia waovu "Hakuna wanachokisubiri ila ni kiama ambacho
kitawakuta Ghafla".
Inshaallah nisiwaboe kusoma ila hivyo ndivyo jinsi ya kutafsiri
ndoto.... Kesho nitawaelezea maana ya kuota manabii... Ingawa kizazi cha
sasa imekuwa ngumu sana mtu kuota nabiii yeyote yule..
Ahsante
JibuFutaNimeota nafanya mapenzi na binamu yangu nisie mjua
JibuFutaNimeota nafanya mapenzina binam ninayemfahamu naomba unitafsirie tafadhali
JibuFuta