MUDA UPI NI SAHIHI KWA MAMA ALIETOKA KUJIFUNGA KUFANYA MAPENZI.
Mama alietoka kujifungua ,anahitaji kujipa mda ili aweze kushiriki
tena tendo la ndoa.Sababu kunauwezekana mkubwa wa kujitonesha kidonda au
kufumuka kwa nyuzi kwa wale walio jifungua kwa operation(caeserean) au
walio ongezewa njia ukeni.
Mama aliejifungua kwa njia ya kawaida.
Njia ya kawaida haina matatizo mengi ,mama atasubiri baada ya wiki
3-4 akajisikia yupo sawa anaweza kuanza kushiriki tendo la ndoa.
Mama aliejifungua kwa c-section(operation)
Unatakiwa kuwa makini sana ongea na mzazi mwanzako,mweleweshane
unahitaji msubirie kidonda kipone kwa ndani na nje ndio muweze kukutana
tena kimwili . Utaepuka kujitonesha kwenye milango ya uzazi ,baada ya
wiki 4-6 mshono utakuwa umekauka na kujifunga vizuri hapo unaweza fanya
tendo la ndoa.
Kwawale walio jifungua kwa njia ya kawaida wakaongezewa njia nao wanahitaji mda ili kidonda kipone wiki 4-6.
Epeka mimba zisizo tarajiwa.
Mama kuwa makini utakapo anza shiriki tendo la ndoa ni rahisi sana
kupata mimba tena. Inakupasa kutumia njia za uzazi iwapo hamjapanga
kuzaa tena kama condom n.k. Ni vizuri mkazaa kwa mpangilio. Baada ya
wiki 6 kjifungua mama anahatari kubwa ya kushika mimba tena kwa
urahisi, japo unaponyonyesha unapunguza kiasi cha kushika mimba ila sio
kwa 100%.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
0656 095 123