Jumanne, 31 Oktoba 2017

Lini Mtoto wako mchanga ataanza Kuona Vizuri? sir ALMASI

Lini Mtoto wako mchanga ataanza Kuona Vizuri??

Lini Mtoto wako mchanga ataanza kuona Vizuri?Mtoto wako ataanza kuona baada ya miezi kumi na mbili, lakini hapa hatakua anaona vizuri kabisa mpaka afikishe umri wa miaka mitatu mpaka mitano.
Uwezo wa mtoto kuona hukua taratibu kwenye mwaka wake wa kwanzaLini Mtoto wako ataanza kuona Vizuri.
Mtoto wako ataanza kuona baada ya miezi kumi na mbili, lakini hapa hatakua anaona vizuri kabisa mpaka afikishe umri wa miaka mitatu mpaka mitano.
Uwezo wa mtoto kuona hukua taratibu kwenye mwaka wake wa kwanza. Wakati ni mchanga mtoto anaweza kuona mwanga na anaweza kutengeneza nyuso mbali mbali. Baada ya mwezi mmoja baada ya kuzaliwa mtoto anaweza kumungalia mama yake uso kwa uso machoni na kuweza kugundua vitu ambavyo vipo umbali wa inch 12.
Mtoto akifikisha miezi 3 au 4 anaweza kutofautisha vitu mbali mbali na kuwa na uwezo wa kuangalia vitu vidogo vidogo vilivyo karibu yake. Jinsi anavyozidi kukua ndio uwezo wake wa kuona unazidi kukua na anaweza kuona vitu vilivyo umbali wa mita 3 na kuangalia shughuli zinazoendelea karibu yake. Kama utakua unafanya kazi karibu yake utamuona anakufata kwa macho na kugeuza geuza kichwa chake.
Kama mtoto wako hawezi kuangalia vitu vinavyo sogea sogea au shughuli zinazoendelea mbele yake, au anapata shida kuangalia kwenye macho yake akiwa ameshafikisha umri wa miezi minne basi inabidi ukamuone dakitari. Inabidi akangaliwe ili ujue nini tatizo.Wakati ni mchanga mtoto anaweza kuona mwanga na anaweza kutengeneza nyuso mbali mbali. Baada ya mwezi mmoja baada ya kuzaliwa mtoto anaweza kumungalia mama yake uso kwa uso machoni na kuweza kugundua vitu ambavyo vipo umbali wa inch 12.
Mtoto akifikisha miezi 3 au 4 anaweza kutofautisha vitu mbali mbali na kuwa na uwezo wa kuangalia vitu vidogo vidogo vilivyo karibu yake. Jinsi anavyozidi kukua ndio uwezo wake wa kuona unazidi kukua na anaweza kuona vitu vilivyo umbali wa mita 3 na kuangalia shughuli zinazoendelea karibu yake. Kama utakua unafanya kazi karibu yake utamuona anakufata kwa macho na kugeuza geuza kichwa chake.
Kama mtoto wako hawezi kuangalia vitu vinavyo sogea sogea au shughuli zinazoendelea mbele yake, au anapata shida kuangalia kwenye macho yake akiwa ameshafikisha umri wa miezi minne basi inabidi ukamuone dakitari. Inabidi akangaliwe ili ujue nini tatizo.

Hiki ndicho alichokiandika Lazaro Nyalandu:




Hiki ndicho alichokiandika Lazaro Nyalandu:

NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017. HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.

AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.

VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.

MIMI Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA, kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.

HIVYOBASI, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM


HISTORIA YAKE:

Lazaro Nyalandu alizaliwa Agosti 18, 1970 mkoani Singida.

Nyalandu alipata elimu ya msingi katika shule za Pohama na Mrumba zilizoko kijijini kwao huko mkoani Singida na kuhitimu mwaka 1987. Aliendelea na masomo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Kibaha mkoani Pwani (1988 – 1991) na alifaulu vizuri na kujiunga na Shule ya Sekondari Ilboru ambako alisoma kidato cha tano na sita.

Wakati akiwa mwanafunzi wa sekondari, Nyalandu alikuwa kiongozi wa juu wa Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania (Ukwata) 1991 – 1993 na baadaye alikuwa miongoni mwa vijana wa Kitanzania walioteuliwa kuzuru jiji la Rio De Janeiro, Brazil na kushuhudia mkutano wa Mazingira mwaka 1993.

Nyalandu alipata elimu yake ya Chuo Kikuu nchini Marekani ambako alihitimu Shahada ya kwanza ya Sanaa katika Usimamizi wa Biashara (BBA) mwaka 1997 katika Chuo Kikuu cha Wartburg.

Kabla ya hapo alikuwa amepata Shahada ya Biashara ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Wardorf nchini humo. Kiongozi huyu, sasa ana Shahada ya Uzamili aliyoipata kwa njia ya utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Buckingham, Uingereza akifuzu katika masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diplomasia.

Baada ya kuhitimu masomo yake ughaibuni, Nyalandu alianza kazi huko huko Marekani katika Benki ya North West, akifanya kazi katika kitengo cha operesheni za kibenki kati ya mwaka 1998–1999.

Aliporejea nchini Tanzania alifanikiwa kuwa sehemu ya washauri wa mke wa aliyekuwa Rais Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa, katika uendeshaji wa taasisi ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).

Ushauri wa timu yake ulisaidia taasisi hiyo kupata misaada mingi kutoka nchi za Ulaya, Marekani, China na nyinginezo. Pia, alikuwa anamsaidia mama huyo katika uandishi wa hotuba zake pale alipokuwa na majukumu makubwa ya kitaifa na kimataifa.

Nyalandu amemwoa mrembo wa Tanzania mwaka 2004 ‘Miss Tanzania’, Faraja Kotta na wana watoto wawili, Sarah na Christopher.


MBIO ZA UBUNGE:

Tangu alipokuwa kijana mdogo, Nyalandu alionyesha kila dalili kuwa na nyota ya uongozi. Watu wanaomfahamu hawakushangaa walipomwona mwaka 2000 anaingia kwenye mpambano ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akilisaka jimbo la Singida Kaskazini. Kutokana na udhaifu wa upinzani uliokuwepo wakati huo alijua atakuwa na kazi kubwa ndani ya chama chake tu, hivyo, alipopitishwa na CCM akapambana majukwaani na wapinzani na kuwa mbunge.

Mwaka 2005, Nyalandu alipitishwa tena na chama chake kuwania ubunge Singida Kaskazini, akakutana tena na upinzani dhaifu kutoka kwa Kimia Omari Rashid wa Chadema, akajivunia asilimia 93.5 ya kura zote na kuwa mbunge hadi mwaka 2010.

Baada ya kupata uzoefu wa ubunge, kwa miaka kumi, Nyalandu alirudi tena kutetea mara ya tatu; CCM ikampa nafasi mwaka 2010 na wananchi wakamchagua kwa ushindi wa asilimia 87.7 akimshinda kwa mara nyingine mgombea yuleyule wa Chadema wa mwaka 2005.

Ushindi wa mara hii ulikuja na bahati kubwa kwa Nyalandu. Bahati ya kwanza ilikuwa kukwea ngazi zaidi. Rais Jakaya Kikwete alimteua Nyalandu kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Novemba 2010 na alidumu hapo hadi Mei 2011 alipohamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, nafasi aliyokaa kwa takriban miaka mitatu.

Bahati ya pili, Januari 2014, nyota yake ilipaa zaidi akapewa wadhifa mkubwa; mara hii akiteuliwa kuwa waziri kamili wa Maliasili na Utalii, sekta ambayo ina changamoto kubwa sana hapa nchini na sekta hiyo nyeti ambayo imenufaisha mamia ya nchi duniani huku Tanzania watu wengi wakisema utalii haujalisaidia taifa kwa kiasi kinachofaa.

MBIO ZA URAIS:

Nyalandu aliweka wazi nia yake ya kuwania urais Desemba 28, 2014 na alitangaza nia hiyo ya kugombea urais katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Ilongero, katika jimbo analoliongoza, Singida Kaskazini, wakati akihutubia mamia ya wananchi.

Katika mkutano huo alisisitiza kuwa “sasa ni zamu ya vijana kuongoza nchi” huku akiwaambia wananchi kuwa safari yake ya ubunge kwa miaka 15 inaanzisha safari nyingine bila kuwaeleza ikiwa bado ana nia na ubunge au la. Aliambatana na mkewe, watoto wake pamoja na wazazi wake.

Kabla ya kutangaza nia ya urais, Nyalandu aliwahi kusikika akisema kuwa “…siwezi kutangaza kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao bila kutumwa na watu” lakini kabla watu wenyewe hawajamtuma aliibuka na kuwaita yeye mwenyewe mkutanoni na kuweka nia yake.

Jumapili, 23 Julai 2017

Mfadhaiko (Depression) Ni Nini?




Mfadhaiko (Depression) Ni Nini?





Maana Ya Mfadhaiko Wa Akili (Depression)

Kila mmoja wetu ameshapata kuwa na huzuni wakati fulani, ni kitu cha kawaida kinachotokea wakati umepotelewa na kitu, kutokana na mihangaiko ya maisha au kutokana na kudharauiliwa. Huzuni ikizidi na ikienda kwa siku nyingi mfululizo (wiki mbili au zaidi) na ikiambatana na hali ya kujiona kuwa si wa thamani tena, kwamba ni mtu usiye na msaada wo wote – basi hii inaweza kuwa ni zaidi ya huzuni. Unaweza kuwa umepata tatizo la kiafya – mfadhaiko, ugonjwa ambao kwa bahati nzuri una tiba.
Mfadhaiko ni ugonjwa unasababisha mtu kuwa na huzuni kila wakati na kukosa hamu ya kufanya vitu au kutenda yale aliyopenda sana kufanya zamani. Mfadhaiko ni ugonjwa unaoathiri namna mtu anavyojisikia, anavyofikiri na tabia yake.
Chanzo halisi cha ugonjwa huu bado hakijafahamika. Wataalamu wanasema kuwa ni muunganiko wa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na urithi, mazingira ya maisha, mambo ambayo mtu amekutana nayo katika maisha na sababu za kisaikolojia. Mtu anaweza kukutana na jambo moja tu kubwa na baya katika maisha yake kama kufiwa na mtu wa karibu, mahusiano mabaya ya ndoa ua kubakwa na akapata mfadhaiko.
Mtu mwenye mfadhaiko hupungukiwa na uwezo wake wa kutenda kazi kiasi kwamba yeye na walio karibu naye wote huathirika.
Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wanaokunywa sana pombe au kutumia madawa ya kulevya. Watu wanaoishi na virusi vya ukimwi, wenye magonjwa ya moyo, waliopatwa na kiharusi, wenye kansa, kisukari, ugonjwa wa Parkinson’s na baadhi ya magonjwa mengine huwa kwenye hatari kubwa ya kupatwa na mfadhaiko. Mtu mwenye mfadhaiko pamoja na magonjwa hayo mengine huwa kwenye hali mabaya zaidi ya kiafya na hupata shida zaidi kuutibu ugonjwa huu.
Utafiti wa zamani ulisema kuwa watu wenye matatizo ya mfadhaiko waliathirika kutokana na kutengwa na jamii, lakini utafiti wa hivi karibuni umetoa majibu tofauti na kuonyesha kwamba mtu anatengwa na jamii kutokana na mfadhaiko alio nao.
Mfadhaiko ni ugonjwa ambao umefahamika toka zamani sana. Hippocrates aliuita ugonjwa huu Melancholia.
Watu wengi mashuhuri wameumwa ugonjwa huu na wengine katika maisha yao yote. Abraham Lincoln, raisi wa 16 wa Marekani na Winston Churchil wa Uingereza ni baadhi ya watu walioumwa ugonjwa huu katika maisha yao yote.

Aina Za Mifadhaiko Wa Akili


Tatizo hili la kuwa na mfadhaiko linakuja kwa namna nyingi. Hapa chini ni baadhi ya aina za mfadhaiko:
Major depressive disorder (major depression
Mgonjwa mwenye aina hii ya mfadhaiko anakuwa na mchaganyiko wa dalili nyingi za mfadhaiko ambazo zitamfanya ashindwe kulala, kusoma, kufanya kazi, kula na kufaidi vitu ambavyo awali vilikuwa vinamvutia sana. Aina hii ya mfadhaiko humpotezea kabisa mgonjwa uwezo wa kushiriki kwenye shughuli za kazi vizuri. Watu wengine hupatwa na hali hii mara moaja wakati wengine hurudiwa mara nyingi.
 Dysthymic disorder (dysthymia)  
Mgonjwa wa aina hii ya mfadhaiko anaweza kuwa na ugonjwa huu kwa muda mrefu, pengine miaka kadhaa, lakini hana dalili ambazo ni kali sana kama za aina ya kwanza hapo juu. Mgonjwa hufanya kazi zake ingawa si kwa ufanisi mkubwa na huwa si mtu mwenye raha kamili. Watu wengine hupatwa na hali hii mara moja tu katika maisha yao wakati wengine hurudiwa mara nyingi. Mgonjwa wa aina hii ya mfadhaiko huweza kupatwa na aina ya kwanza hapo juu mara moja au zaidi katika maisha yake.
  Psychotic depression
Endapo mfadhaiko utakuwa mkubwa na kuambatana na mtu kuwa na maluweluwe (hallucinations) na kuwa nje ya maisha halisi, mtu huyu anaweza kuwa na aina ya mfadhaiko unaoitwa Psychotic depression, ugonjwa ambao mara nyingine huitwa delusional depression.


Postpartum depression (postnatal depression)
Kama mama mzazi atapatwa na mfadhaiko wiki chache baada ya kujifungua, anaweza kuwa amepatwa na postnatal depression. Wataalamu wanasema kuwa asilimia 15 hadi 20 ya akina mama hupatwa na ugonjwa huu baada ya kujifunga, bahati mabaya ni kwamba wengi hawagunduliki na wanateseka kwa miaka mingi baada ya kujifungua. Mama anaweza kuupata ugonjwa huu muda wo wote katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya kujifungua.
SAD (seasonal affective disorder)
Idadi ya watu wanaopatwa na ugonjwa huu huoongezeka zaidi kadiri unavyokwenda mbali zaidi na Ikweta. Mwisho wa kipindi cha summer ni mwanzo wa kuona jua kwa muda mfupi zaidi au mwanzo wa saa nyingi zaidi za giza kwa siku. Mtu anayepatwa na mfadhaiko katika kipindi hiki huweza kuwa amepeta aina hii ya ugonjwa. Ugonjwa huu hutoweka wenyewe wakati wa spring au summer.
Bipolar disorder (manic-depressive illness)
Ugonjwa hauonekani kwa wingi kama aina nyingine za hapo juu. Tabia kuu ya aina hii ya mfadhaiko ni kuwa na vipindi vya dalili kuwa juu sana na baadaye kushuka. Viwango hivi vya juu na chini huitwa manias.


Dalili Za Kuwa Na Mfadhaiko

  • Kutopenda kushirikiana na watu wengine
  • Kuwa na huzuni kila wakati na kujiona kuwa ni mtu usiyefaa
  • Kukosa mwamko na hamu ya kufanya shughuli
  • Matatizo katika kufanya maamuzi
  • Kutotulia na kuwa na hasira
  • Kula zaidi au pungufu ya kawaida
  • Kulala zaidi au pungufu ya kawaida
  • Kushindwa kutuliza mawazo kwenye jambo
  • Matatizo ya kumbukumbu
  • Kutotulia na kuwa na hasira
  • kukosa raha ya maisha
  • Kukosa hamu ya kuanya mambo uliyoyapenda sana zamani na         hamu ya kufanya mapenzi
  • Kujisika vibaya juu yako au kuwa mwenye makosa
  • Kuona kwamba huwezi kutatua matatizo yako ya maisha
  • Kuumwa kichwa kubanwa misuli, matatizo ya uyeyushaji chakula tumboni, matatizo ambayo hayaponi kwa kutumia dawa
  • Kuwa na mawazo ya kujiua

Jinsi ya kutafsiri ndoto uliyoota

Katika Uislamu tumeambiwa Ndoto ni sehemu ya unabii tulioachiwa, pia uislamu unaeleza aina kuu mbili za ndoto yaani Ndoto zinazotokana na shetani na ndoto inayotoka kwa mwenyezi mungu.

Pia Uislamu umeeleza ndoto ya kweli uotwa muda gani (Mfano amesema bwana Mtume, ndoto yeyote atakayeota muumini kabla ya swala ya alfajiri, ndoto hiyo ni ya kweli), kwa ufupi ndoto ya kweli ni ile mtu anayeota usiku wa manane akiwa hana msongamano wa mawazo na wala huna janaba la hawala.

Uislamu umesema kuwa kama mmoja wenu ameota ndoto nzuri basi amfuate mmoja wenu anayejua na amweleze ili apate maana yake. Kama uislamu umeelezea vizuri kuhusu ndoto Je ndoto hutafsiriwaje?..

Kwa ufupi kuna watu wengi wanadai wana uwezo wa kutafsiri ndoto, ukweli ni kuwa utafsiri wa ndoto ni ngumu sana na hakuna mtu anyejua kutafsiri ndoto zote ukiondoa manabii ambao kwa sasa hawapo tena. Wengi wanaishia kudanganya maana halisi ya ndoto, kumbuka uislamu umesema, "KAMA MMOJA WENU AKIOTA NDOTO CHAFU NA MBAYA BASI ASIITANGAZE, MAANA NDOTO HIZO ZIMETOKA KWA SHETANI".

Leo nitawafundisha jinsi ya kutafsiri ndoto ili msije mkadanganywa na mtu lakini tafsiri nitakayowapa ni Based on Islam na sio dini nyingine, japokuwa baadhi ya ndoto inabeba maana sawa kwa muislamu na siye muislamu. Kama wanavyotafsiri wanazuoni wengine..

Ukiota ndoto yoyote katika wakati ulioelezwa basi angalia hiyo ndoto kama inafanana na Aya yeyote ya Kuran anu Hadith Yeyote ya Bwana Mtume PBUH. Hiyo itakuwa ndio maana yake:-

Mfano 1: Umeota umetumbukizwa kwenye Kisima, tafsiri yake ni surat Yusuf... Yaani Ndugu zako wanataka kukutendea uadui, lakini kwa uwezo wa Mwenyezi mungu hawatafanikiwa wanavyotaka na utakuja kuwa na uwezo wa mali na mamlaka kuliko wao.

Mfano wa Pili: Umeota ndege amekudondoshea jiwe kichwani, Tafsiri yake Surat fil... Unaonywa kuwa unafanya yaliyovuka mipaka hivyo utaangamia.

Mfano wa tatu:
Umeota Ndege anaokuambia kitu, Tafsiri yake ni surat Naml.. Habari anayokuambia ni ya kweli hivyo unatakiwa uifanyie kazi haraka.

Mfano wa nne: Umeota unakurupuka na ukaambiwa kiama!, watu wengi wanakwenda wasipopajua, Tafsiri yake ni kuwa unapewa Onyo kuna jambo linalomchukiza Mungu unalifanya acha mara moja. kumbuka pale allah aliposema kuwaambia waovu "Hakuna wanachokisubiri ila ni kiama ambacho kitawakuta Ghafla".

Inshaallah nisiwaboe kusoma ila hivyo ndivyo jinsi ya kutafsiri ndoto.... Kesho nitawaelezea maana ya kuota manabii... Ingawa kizazi cha sasa imekuwa ngumu sana mtu kuota nabiii yeyote yule..
  BY ALMASI

happy birthday sir ALMASI MICHAEL 23/JULY







Jumapili, 7 Mei 2017

35 killed in school minibus crash in Tanzania






Thirty-two schoolchildren, two teachers and a minibus driver where killed in Tanzania when their vehicle plunged into a roadside ravine in the northern tourist region of Arusha on Saturday, a senior police official said."The accident happened when the bus was descending on a steep hill in rainy conditions," Arusha regional police commander Charles Mkumbo told Reuters by telephone."We are still investigating the incident to determine if it was caused by a mechanical defect or human error on the part of the driver."

The students killed in the accident, which occurred at about 9:30am in Karatu district, were standard seven pupils, aged 12 to 13, from the Lucky Vincent primary school on their way to visit another school, Mkumbo said.

President John Magufuli described the accident as a "national tragedy" in a statement.Tanzania, the second-largest economy in east Africa, has a poor road safety network, but buses remain the main form of public transport between towns.

More than 11,000 people were killed in road accidents in Tanzania between 2014 and 2016, according to government data.