Aina za wanaume kwa mujibu wa dini ya Kiislam.
Huyu ni hatari kwa sababu hatokuwa na ujasiri wa kumkemea mke pale anapokosea kwa kuhofia mke asije kasirika na kusitisha huduma ya kuilisha familia.
2-ADHWWAAQ(ONJAONJA)
Huyu ni mwanaume anayependa kuoa na kuacha bila ya sababu, huyu ni hatari kwa sababu anazichezea sheria za Allah na kuwadhalilisha wanawake, talaka inakubalika katika Uislamu lakini imewekwa katika nafasi ya mwisho ikiwa hatua zote muhimu zimeshindikana. Kuoa na kuacha bila ya sababu za msingi hakukubaliki katika Uislamu.
3-ALMANNAAN.
Huyu ni mwanaume anayemnunulia mkewe vitu vya aina mbalimbali kisha anaanza kujitangaza nje.
Huyu ni mtu hatari kwa sababu kitendo cha kumpa mtu kitu kisha ukaanza kujitangaza kinaharibu malipo na kinathibitisha kwamba lengo lake lilikuwa si kupata radhi za Allah bali ni kutafuta sifa kwa watu.
4-ADDUYUUTH(ASIYE NA WIVU)
Huyu ni mwanaume aliyeridhia mkewe achezewe na wanamume wengine au Mkewe aoneshe mapambo yake kwa wanaume wengine. Na hili tunalishuhudia katika jamii utakuta mwanamume anamruhusu mke atoke ndani ya nyumba akiwa amevaa mavazi yasiyostiri mwili hatimae anawapa mtihani wale wanaume barabarani. Asiyekuwa na wivu haingii peponi.
5 ALMUTAFAHHISH(MWENYE MANENO MACHAFU)
Huyu ni Mwanamume ambae anapokorofishana na mkewe hukimbilia kutoa maneno machafu kama vile kumwita mke “Mbwa”Nguruwe”nk.
6-ALJAAHIL (MJINGA)
Huyu ni Mwanaume asietaka kujifunza mambo ya dini yake, na kwa ajili hii utakuta hamudu kuilea familia katika maadili anayoyaridhia Allah mtukufu.
7-ALMUSRIFU.
Huyu ni mwanaume mwenye kutumia pesa yake na vitu vingine kwa fujo khaswa pale anapopokea mshahara wake.
Israafu katika matumizi ni haramu.
8-ALMUSHRIK (MSHIRIKINA)
Huyu ni mwanaume ambae ameiweka mbele shirki katika mambo yake hata mtoto wake akiumwa MALARIA atampeleka kwa mganga wa kienyeji. Huyu hafai kabisa kwa sababu anachokifanya ni kitu kizito na akifa kabla ya kutubia atastahiki kuishi milele Motoni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
0656 095 123