Jumamosi, 3 Septemba 2016

historia ya wachaga - almasi



WACHAGA
Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu lakini pia mchanganyiko wa damu, hasa ya Kikushi wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlimaKilimanjaro, mkoani Kilimanjaro.
Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara, kilimo na kazi za maofisini.
Wachagga ni kabila la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania.[1] Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga 2,000,000.
·         1Vikundi vya Wachagga
·         2Lugha ya Kichagga
·         3Koo za Kichagga
·         4Utawala wa jadi wa Wachagga
·         5Elimu kati ya Wachagga
·         6Ardhi
·         7Kilimo na chakula
·         8Maoni juu ya Wachagga
·         9Tanbihi
·         10Marejeo
·         11Viungo vya nje
Vikundi vya Wachagga[hariri | hariri chanzo]
Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na ya maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la Kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogomadogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia mashariki (Tarakea, Rombo) hadi magharibi kwa Kilimanjaro (Siha, Machame).
Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Vunjo ambao wanajumuisha watu wa Mwika, Mamba, Marangu, Kilema na Kirua ambayo ndio inajulikana na wengi kama Kirua Vunjo. Ukipenda unaweza kuwagawa watu hawa wa Vunjo kama Wa-Mwika, Wa-Mamba ,Wa-Marangu,Wa-Kilema,na Wakirua.Makabila mengine ni Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, na Wa-Machame, Wa-Uru, na Wa-Siha.
Lugha ya Kichagga[hariri | hariri chanzo]
Lugha ya Kichagga inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha magharibi mwa Kilimanjaro.
Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika Kirombo, Kivunjo, Ki-Old Moshi, Kiuru,Kikibosho, Kimachame, na Kisiha.
Lugha hizo zinakaribia kufanana kadiri makabila hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Kivunjo kinafanana na Ki-Old Moshi. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho.
Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru, Arusha, na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Kimeru. Kwa sababu hiyo Wameru wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo.
Koo za Kichagga[hariri | hariri chanzo]
Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: kwa mfano, familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama ukoo wa akina Mushi, Kimaro, Swai, Massawe, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame.
Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kamnde, Kileo, Kimambo, Tesha, Msaki, Assey, Kyara, Kessy, Ndanu, Macha, Mbishi, Kombe, Njau wanatoka Old Moshi na Vunjo.
Majina mengine ya Old Moshi ni kama yafuatayo: Mmari, Macha, Mshiu, Kyara, Moshi, Massamu, Kimambo, Mboro, Mlngu, Tenga, Njau, Malisa, M aro, Maeda, Ngowi, Lyatuu na mengine mengi.
Kavishe, Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe, Silayo, Lyaruu, Makyao, Mowo, Lamtey, Tairo, Mramba, Kauki wanatoka Rombo.
Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau wanatoka Marangu na Kilema.
Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba, Foya, Munishi, Kilawe, na kadhalika hutoka Kibosho.
Ukoo wa akina Teri wako Mamba, Chami, Chuwa, Kiria Owoya na wachache Sango, Old Moshi na wengine walihamia Maji ya Chai, Mkoa wa Arusha.
Utawala wa jadi wa Wachagga[hariri | hariri chanzo]
Watawala wa Kichagga waliitwa "Mangi". Hawa walihodhi mashamba, ng'ombe na waliheshimiwa kama viongozi wa kikabila. Walikuwa na nguvu za kisiasa nautajiri. Baadhi ya Ma-mangi mashuhuri katika historia ni kama Mangi Rindi aliyeingia mikataba na wakoloni (Wajerumani), Mangi Sina wa Kibosho - anajulikana kwauhodari wake wa vita katika kupigana na Wamachame na kupora ng'ombe na mazao yao, hata mpaka leo makabila ya Kimachame na Kikibosho hayaoani kwa urahisi, na Mangi Marealle wa Marangu na Vunjo. Mangi Meli huyu alikuwa mangi wa waoldmoshi ambaye alipigana na wajerumani na aliishia kukatwa kichwa na mpaka sasa kichwa chake kipo ujerumani alizikwa kiwiliwili tuu baada ya kumnyoga na mti aliyonyongewa upo mpaka sasa sehemu ya oldmoshi bomani karibu na kolila sekondari .
Wakoloni walipokuja Kilimanjaro waliingia mikataba na viongozi hawa wa kikabila ili kuweza kuweka misingi yao ya kikoloni. Pia ndugu na watoto wa Ma-mangi walikuwa wa kwanza kupata elimu ya kikoloni, kwa hiyo waliweza kushirikishwa katika serikali za kwanza. Hawa pia wanaaminika walikuwa kama mabepari wa kwanza wa kijadi, maana walifanyiwa kazi na watu wengine wakati wao Ma-mangi wamekaa kuhesabu mali zao.
Usemi maarufu wa "u-Mangi-meza" nadharia inawezekana kuwa umetokana na watawala hawa wa Kichagga.
Elimu kati ya Wachagga[hariri | hariri chanzo]
Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa wa kufanya biashara na pia kilimo. Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo Wamisionari wa Ukristo walijenga makanisa na shule.
Sababu hii imefanya Wachagga kuwa kabila lenye watu wengi zaidi walio na elimu ya kisasa na mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa idadi ya shule za sekondarinchini Tanzania. Kulingana na takwimu za elimu mkoa wa Kilimanjaro una shule za sekondari zaidi ya 320. Pia mkoa una shule za msingi zipatazo 950. Idadi hii ya shule ni kubwa zaidi ya idadi ya shule katika mikoa mingine Tanzania.
Shule nyingi za sekondari ziko katika mkoa huu kwa sababu zifuatazo: 1) Hali ya hewa na vivutio vya kitalii katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakolonina kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamisionari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za wakoloni 2) Serikali ya Tanzania ilirithi shule zilizojengwa na wakoloni 3) Wachagga waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa shule binafsi kama kitega-uchumi, wakati wakazi wa mikoa mingine kadhaa walisubiri serikali iwajengee shule. 4) Ukichanganya sababu 1, 2 & 3 utagundua shule katika mkoa Kilimanjaro zimezidi sana idadi ya shule katika mikoa mingine yote.
Ni vema pia kusema kuwa shule hizo huvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi Wachagga tu.
Ardhi[hariri | hariri chanzo]
Ingawa ardhi ni msingi wa maendeleo kwa watu wote, kwa Wachagga, ardhi ni mali sana kwa sababu kilimo chao ni cha mazao ya kudumu kama kahawa na ndizi hukaa shambani kwa muda wa miaka mingi.
Mojawapo ya urithi wapewayo watoto ni "kihamba". Hii ni sehemu ya ardhi ambayo mtoto anategemewa atajenga na kuanzisha familia yake. Bahati mbaya watoto wa kike walikuwa hawapewi kipaumbele katika ugawanaji wa vihamba. Uhaba wa ardhi huko Uchaga ulipelekea Wachagga wengi kuhamia mikoa mingine. Hivi leo utakuta Wachagga wakiishi Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya n.k. wakiwa wamepanda migomba yao na kuendesha biashara za maduka ya vyakula.
Ukienda kwenye mikoa hiyo utakuta wamejenga jamii zao na vyama vyao vya kusaidiana wakati wa sherehe au matatizo. Aidha hata pombe ya mbege utaweza kuikuta kwenye makusanyiko ya Wachagga katika mikoa mbalimbali.
Kilimo na chakula
Wachagga hulima mazao ya chakula kama vile mahindi, maharagwe, viazi, ndizi, ulezi na mboga mbalimbali. Pia mazao ya biashara kama vile kahawa, nyanya navitunguu.
Ndizi za Wachagga[hariri | hariri chanzo]
Ingawa Wachagga wa leo wanakula vyakula mbalimbali kama vile ugali, wali na viazi, chakula kikuu cha Wachagga ni ndizi.
Kuna ndizi za aina mbalimbali na kwa matumizi tofauti. Mfano ndizi sukari ni fupi na huachwa hadi ziive na huliwa mbivu kama tunda.
Ndizi mshale hukatwa zikiwa mbichi na kupikiwa vyakula mbalimbali pamoja na nyama ya ng'ombe, kondoo au mbuzi. Mara nyingine hupikwa na maharage,choroko, kunde au hata maziwa ya mtindi. Vyakula vya ndizi huja kwa ladha tofauti kama vile ndizi nyama, mtori, machalari, kiburu na kadhalika.
Aina nyingine ni ndizi ng'ombe ambazo huachwa ziive halafu humenywa na kutumiwa kutengenezea pombe maarufu iitwayo mbege. Mbege hutengenezwa kwa kutumia ndizi mbivu, maji, na ulezi.
Aina nyingine ni ndizi mzuzu. Hizi zikikomaa huachwa zianze kuiva kidogo halafu huchomwa na kuliwa kama kitafunwa pamoja na chai au pombe. Ukipita mitaa yaDar es Salaam utaona ndizi mzuzu zikichomwa sambamba na muhogo au kuku vumbi au kiti moto.
Wachagga na muhogo[hariri | hariri chanzo]
Inasemekana kuwa "Mchagga halisi hali muhogo - akila muhogo atakufa". Usemi huu umetokana na historia ya mababu kuwa Wachagga waliopanda mihogo Kilimanjaro enzi za kale walikufa baada ya kuila. Historia hiyo yaweza kuwa ya ukweli kwa sababu aina nyingi za mihogo zinajenga sumu ya sianidi ndani yake; watu waliozoea kutumia mihogo huwa na njia za kuondoa sumu kwa kuiloweka mihogo katika maji kwa muda. Lakini kama Wachagga wale wa zamani, hasa wa Machame, walifanya jaribio bila kujua mbinu ya kuondoa sumu, ajali iliweza kutokea. Cha kushangaza ni kwamba hukohuko Kilimanjaro, majirani na watani wa Wachagga, yaani Wapare, walikuwa wameshazoea mihogo na ilikuja kuwa moja ya chakula chao kikuu.
Ulaji kiti-moto[hariri | hariri chanzo]
Pamoja na kilimo cha mazao, Wachagga hupendelea sana kufuga nguruwe. Tabia ya kula nyama ya nguruwe ijulikanayo leo kwa jina la "kiti moto" ni moja ya mambo yaliyoenezwa na Wachagga. Ulaji wa "kiti moto" haukuwa pendeza baadhi ya wenyeji wa Pwani kama Dar es Salaam ambapo Wachagga walihamia, kwani wakaaji wengi wa Pwani ni Waislamu kwa hiyo nguruwe kwao ni haramu. Wakazi wa Dar es Salaam watokao makabila mengine na wasiyo Waislamu kwao kula nguruwe ilikuwa "ruksa".
Maoni juu ya Wachagga[hariri | hariri chanzo]
Ingawa wanaume wa Kichagga hupendelea kufanya kazi mbali na kwao, wake zao hukaa nyumbani (Moshi) na hufuga ng'ombe na kazi za shambani. ila kwa sasa kutokana na ugonjwa wa ukimwi tabia hii imepungua miongoni mwao.
Wanawake wa Kichagga (hasa kutoka Machame) hujulikana kama wafanyakazi hodari. Huchangia sana katika mapato ya nyumbani na chakula.
Ingawa kipato cha Wachagga ni kikubwa kulingana na cha makabila mengine, takwimu zinaonyesha watoto wa mkoa wa Kilimanjaro kuongoza kwa utapiamlo. Sababu kubwa ya watoto kuwa na utapiamlo ni wazazi kujali zaidi kazi kuliko muda wa kuwahudumia watoto.
Wengi wa watoto hao ni wale ambao wazazi wao ni watu wa pombe na kipato chao kinaishia kilabuni. Utaona kwamba Uchagga una vilabu vingi vya pombe na vinaongezeka kwa sababu imekuwa biashara kubwa. Karibu kila kaya kumi na tano kuna kilabu cha pombe na kiwango cha chini kabisa cha pombe inayouzwa kwa siku katika vilabu hivyo si chini ya madebe sita au lita mia moja. Pombe ni sababu moja ya watoto kuwa na utapiamlo.
Hii inawezekana kuwa matunda ya wazazi kutowalisha watoto wao chakula cha kutosha au chakula bora. Kuna sehemu nyingine za Uchagga kama Old Moshi naKibosho ambapo watoto wadogo hupewa pombe ya mbege asubuhi, mchana na jioni.
Sababu nyingine ni kazi; mama wa Kichagga anaweza kushinda shambani kutwa na hana desturi ya kubeba watoto mgongoni kwenda nao shambani, hivyo wanakuwa nyumbani ama wenyewe au na mayaya. Mfano ulio dhahiri ni nyakati za asubuhi na mapema kwenye vyombo vya usafiri karibu robo tatu ya abiria niwanawake wakienda katika shuguli za biashara na kilimo na vivyo hivyo nyakati za jioni wakirudi majumbani. Hao ni nje ya wale wanaotumia usafiri wa miguuambao ni wengi zaidi.
Pia baadhi ya kina mama wa Kichaga wanawajali waume zao zaidi kwani nyama nzuri ni ya baba. Kuepuka gharama baba ataandaliwa chakula kizuri, tofauti na chakula walichoandaliwa watoto, japo ni chakula kilekile.
Pia Wachagga wamekuwa na desturi ya kuwaenzi wazee wao waliotangulia mbele za haki kwa kuwatambikia kwa pombe na nyama za mbuzi pale tu wanaporudi nyumbani ifikapo mwezi Desemba. Hili limekuwa suala la kawaida sana na halipingiki. Wengi wao huwa wanarudi na magari, ndiyo sababu utaona ya kwambwa kila ifikapo mwezi Desemba kila mwaka foleni za magari zimekuwa zikiongezeka kutokana na Wachagga kurudi nyumbani msimu wa sikukuu. Wengi wao wamekuwa wakitoka sehemu mbalimbali za nchi na hata nje ya nchi.
Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu.
Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wamepokea sana dini [imani] ya Ukristo kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa ni kipindi cha likizo kwao, inaaminika pia kuwa kurudi kwao Uchagani wakati wa Krismasi ni pamoja na kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada ya kazinyingi za kutafuta pesa mwaka mzima.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

0656 095 123